THE Revolutionary Government of Zanzibar

Ministry of Education and Vocational Training

MKUTANO WA UTAMBULISHO WA MRADI (MSINGITEK) WA MILELE ZANZIBAR FOUNDATION UNAOFADHILIWA NA IMAGINE “WORLDWIDE”

Naibu Katibu Mkuu Taaluma Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dk Mwanakhamis Adam Ameir Amesema kujua kusoma na kuandika kwa watoto wa darasa la 1 hadi la 3 ni miongoni mwa jitihada za Serikali katika sekta ya Elimu nchini.

Ameyasema hayo wakati akifunguawa mkutano wa Utambulisho wa Mradi (MsingiTEK) wa Milele Zanzibar Foundation unaofadhiliwa na Imagine “WorldWide” unaolenga kumuwezesha mtoto kujua kusoma na kuandika kupitia mfumo wa Teknolojia hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi ya Afisa elimu Wilaya Skuli ya Tumekuja Sekondari Mjini- Unguja.

Amesema idara zote za wizara ya Elimu ni lazima zisimamie jitihada hizo kwa kuhakikisha Lego Hilo linafikiwa kwa wakati.

Aidha Dk.Mwanakhamis Amewasisitiza walimu wakuu wawajibike kupitia huu mradi ili waweze kuhamasisha kwa walimu wa masomo waengeze ubunifu kuwasaidia watoto wasome kwa bidii

Mapema Afisa Mdhamin Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Ndugu Moh’d Nassor Salim ameipongeza Milele Zanzibar Foudation kwa hatua nzuri iliofikia katika kusaidia sekta ya Elimu nchini.

Pia amewasisitiza Maafisa Elimu Wilaya kushirikiana kwani ndio chanzo cha mafanikio katika maendeleo.

Mradi huo unalengo LA kuimarisha upatikanaji wa elimu bora , kwa kuzingatia ujuzi wa msingi, STEM (Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Mahesabu), na Sanaa.