
Katibu Mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Ndugu Khamis Abdulla Said amewapongeza na kuwatunuku vyeti wanafunzi wa skuli ya Leera kwa kushinda katika mashindano ya TCRO 2026.
Akizungumza katika hafla hiyo leo tarehe 10 Agosti 2026 Katibu Khamis amesema hatuwa waliyoionesha wanafunzi hao inadhihirisha kuwa elimu inayotolewa Zanzibar ni ya viwango bora ambapo inaendelea kukuwa kila siku.

Amesema serkali inaendelea kuimarisha sekta ya elimu ambapo matarajio yake ni kuzalisha vijana walio wabunifu, wavumbuzi, watafiti na wajasiriamali wa teknolojia ili waweze kuendana na mabadiliko ya dunia na kukidhi katika soko la ajira duniani.
Nao walimu wa skuli hiyo wameeleza kuwa hatua ya mafanikio hayo inatokana na ushirikiano wa karibu kati ya walimu na wazazi Pamoja na jitihada za wanafunzi katika masomo yao.
Mashindani hayo ya midahalo na uwezo wa kuzungumza katika hadhara yaliyoandaliwa na TCRO yamejumuisha zaidi ya wanafunzi 200 kutoka nchi 15 ambapo kwa upande wa skuli ya Leera wamepata medani za dhahabu 9.
Imetolewa na Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano _ (WEMA)