
19 Julai, 2026
Uwanja wa Ndege – Abeid Amani Karume, Unguja
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ndugu Khamis Abdulla Said, kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar (ZHESLB), Ndugu Umrat Suleiman Mohamed, leo wamewapokea kwa heshima wahitimu wa American University of Ras Al Khaimah kutoka Falme za Kiarabu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Unguja.
Wahitimu hao wamefanikiwa kumaliza masomo yao kupitia ufadhili wa masomo (Scholarship) ulioratibiwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar (ZHESLB) kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa Ras Al Khaimah.
Mafanikio ya wahitimu hawa ni ushahidi wa dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuendelea kuwekeza katika elimu kama nyenzo muhimu ya kujenga rasilimali watu yenye ujuzi, maarifa na uwezo wa kuchangia maendeleo endelevu ya taifa.
ZHESLB inaendelea kutekeleza jukumu lake la kuwezesha vijana wa Zanzibar kupata fursa za elimu ya juu zenye ubora, ndani na nje ya nchi, ili kuzalisha wataalamu watakaochangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Zanzibar.
Imetewa na kitengo cha Habari na Uhusiano (WEMA)