
Watendaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakiongozwa na Mkurugenzi wa Elimu Mbadala na watu wazima Ndugu Mashavu Ahmada Faki wakiwa pamoja na ujumbe kutoka Shirika la kimataifa linaloshughulikia watoto duniani (UNICEF) wakiongozwa na Mkuu wa shirika hilo ofisi ya Zanzibar Ndugu Luxmi Bhawani wametembelea miradi ya ZIPOSA iliyopo Mwera Pongwe, Mkoa wa Kusini _Unguja.
Miradi hiyo ni pamoja na Ushoni, kitalu cha miche, kiwanda cha kuchakata taka taka kuwa mkaa na kituo cha ufundi seremali.
Mpango wa vijana rika walionje ya mfumo rasmi wa elimu (ZIPOSA) unafadhiliwa na shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF)
Imetolewa na Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano (WEMA)