
Leo tarehe 01/07/2026, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ndugu Khamis Abdulla Said, amekabidhi pikipiki 600 za aina ya Kodmor kwa Walimu Wakuu wa skuli za Unguja na Pemba.
Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu amesema kuwa lengo la ugawaji wa pikipiki hizo ni kuimarisha utendaji kazi wa Walimu Wakuu kwa kuwawezesha kufuatilia kwa ufanisi shughuli mbalimbali za kila siku za skuli, pamoja na kupunguza changamoto za usafiri zinazoweza kuchelewesha utekelezaji wa majukumu yao.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Imetolewa na Kitengo cha Habari, Uhusiano na Mawasiliano, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.