
Leo tarehe 24 Juni, 2026, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Muhamed Mussa, amezindua Baraza jipya la Taasisi ya Chuo cha Ufundi Karume (KIST) na kuwaaga Mwenyekiti na wajumbe wa Baraza lililomaliza muda wake, katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa KIST, Mbweni, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Waziri aliwashukuru Mwenyekiti na wajumbe waliomaliza muda wao kwa mchango wao mkubwa katika kuimarisha maendeleo ya taasisi hiyo, huku akilihimiza Baraza jipya kufanya kazi kwa weledi, ubunifu na uwajibikaji ili kuendeleza dhamira ya kutoa elimu bora ya ufundi na stadi za kazi nchini.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi, watendaji wa taasisi pamoja na wajumbe wapya na waliomaliza muda wao wa uongozi.