
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhamed Mussa amesema serikali inafanya jitihada mbali mbali ili kuhakikisha watoto wote mijini na vijijini wanapata elimu iliyobora na iliyo sawa.
Akizungumza katika ufunguzi wa kituo cha Maandalizi tutu Mchikichini amesema Maono ya Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi yamebadilisha sekta ya elimu katika maeneo yote ya visiwa vya Zanzibar.
Amefahamisha kuwa serikali imeanzisha mradi jumuishi unaohusisha sekta ya elimu, afya, kilimo, ustawi wa jamii na tawala za mikoa ili kuhakikisha watoto wanakuwa salama na kulindwa katika afya na makuzi yao.
Kwa upande wake meneja wa huduma za jamii kutoka ofisi ya Raisi ya ufuatiliaji na Usimamizi Dkt Ibrahim Kabole amesema kituo hicho kitatoa huduma mbali mbali ikiwemo kutoa nasaha kwa wazazi kuhusu lishe na namna bora ya kuwalea watoto pamoja na kupatiwa chanjo.
Mwakilishi wa UNICEF ndugu Elke Wisch amesema ni jambo jema kuona kituo hicho kinajumuisha huduma mbali mbali kwa ajili ya elimu bora ya mtoto na maendeleo mazuri katika makuzi yao.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Ndugu Khamis Abdulla Said amesema ukarabati wa kituo hicho umegharimu shilingi 160, ambapo awali ilikuwa na madarasa 3 na kwa sasa ni 4.
Imetolewa na Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano (WEMA