
Waziri wa Elimu na Mafunzo Amal Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa ametembelea na kukagua maendeleo ya programu ya MsingiTek katika hatua ya utekekezaji ilipofikia katika skuli ya Msingi K/smaki – Unguja
Huu ni mpango wa kuleta maboresho katika elimu ya awali na msingi kupitia matumizi ya TEHAMA ili watoto waweze kupata stadi muhimu za msingi mapema
Programu hiyo ya MsingiTek inalenga kuboresha teknilojia ya kidijitali katika kuwasaidia watoto kujua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa ufanisi zaidi (KKK) kwa kutumia njia ya (Tablet) vishikwambi (DIGITAL EGRA NA EGMA) kupitia programu ya MsingiTek
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano (WEMA)