
Naibu Katibu Mkuu wa Taaluma katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, , amesema hatua hiyo inalenga kuwawezesha wanafunzi kuhitimu elimu ya lazima wakiwa na ujuzi katika fani mbalimbali utakaowasaidia kujiajiri na kupunguza utegemezi wa ajira za Serikali.
Ameyasema hayo leo, tarehe 18 Mei 2026, wakati alipokutana na ujumbe kutoka Sweden kupitia Sweden Folk High Schools katika ofisi za Wizara ya Elimu iliyopo Mazizini, Unguja.
Dkt. Mwanakhamis amesisitiza umuhimu wa kushirikiana na kwa lengo la kubadilishana uzoefu pamoja na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoweza kujitokeza katika utoaji wa elimu na mafunzo ya amali.
Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Mbadala na Watu Wazima, , ukishirikiana na (KTO) pamoja na , ikiwa ni sehemu ya kukamilisha ziara yao ya mafunzo nchini
Sambamba na hayo, ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea kituo cha Elimu Mbadala na Watu Wazima kwa ajili ya kuona na kujifunza shughuli mbalimbali za amali zinazofanywa na wanafunzi katika kuendeleza ujuzi wao.

Imetolewa na kitengo cha Habari na Uhusiano (WEMA)