
Leo tarehe 09 Aprili 2026, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Dkt. Mwanakhamis Adam Ameir, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) uliofika Zanzibar kwa ajili ya kufanya Tathmini ya Muda wa Kati ya utekelezaji wa Mradi wa SEBEP (Mid-Term Review Supervision Mission).
Lengo la ziara hiyo ni kufanya tathmini ya hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa SEBEP, kubaini mafanikio, changamoto pamoja na kuweka mikakati ya kuendeleza utekelezaji wake kwa ufanisi zaidi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano WEMA.