
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatekeleza mpango wa Compact Pertnership wa mwaka 2023, wenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaokabiliwa na changomoto ya Ujifunzaji, hususan katika stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tisa (9) wa Tathmini ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu Zanzibar kwa mwaka 2025 uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Madinat al Bahri Mbweni Zanzibar.
Amesema Matokeo ya Upimaji wa kujua kusoma, kuandika na kuhesabu ya mwaka 2025, yameonesha wazi kuwa idadi kubwa ya wanafunzi hawajafikia viwango vinavyotarajiwa, hivyo, ipo haja ya kuongeza jitahada zaidi ili kuweze kuitatua changamoto hio.
Amefahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuweka msisitizo mkubwa katika kuimarisha stadi za msingi za ujifunzaji, sambamba na kutambua umuhimu wa stadi za amali yaani ( VOCATIONAL TRAINING ) katika kukidhi mahitaji ya soko la ajira la sasa na baadae ndani na nje ya nchi.
Aidha, Mhe. Hemed amesema Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026 imepanga kujenga madarasa 1,000 ambapo kwa sasa hatua hiyo inaendelea kwa kujenga Skuli za Ghorofa 13, katika maeneo mbalimbali nchini, ili kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani na kuondoa mikondomiwili ya uingiaji skuli kwa baadhi ya skuli ambazo bado zinaendelea na utaratibu huo.
Kadhalika, Serikali imedhamiria kuajiri walimu 1,500 ili kuboresha uwiano wa walimu na wanafunzi jambo ambalo z linaonesha dhamira ya dhati ya Serikali ya kuimarisha obora wa elimu hapa nchini.
Katika Mkutano huo, Mhe. Hemed amewataka washiriki kuendeleza ushirikiano wa karibu zaidi, baina ya Serikali, wadau wa maendeleo, walimu, wazazi na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora yenye kumuwezesha kumudu stadi za msingi na kumjega kwa maisha yake ya baadae.
Amewasihi kuutumia vyema mkutano huo kwa kujadiliana kwa kina, kubadilishana uzoefu, kutoa mapendekezo na suluhisho la kufikia malengo ya kuwa na wanafunzi wenye uwezo wa kujua kusoma, kuandika na kuhesabu wakiwa katika madarada ya awali
Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. LELA MOHAMED MUSSA amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikiekeza fedha nyingi katika sekta ya elimu kwa lenho lw kuimarisha na kuboresha miundombinu ya elimu na kuhakikisha wanafunzi wa Zanzibar wanapata elimu bora.
Mhe. Lela amefahamisha kuwa kufanyika kwa mkutano huo kunatoa fursa kwa wadau mbalimbali wa sekta ya elimu kufanya tathmini ya mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta ya elimu sambamba na kutafuta mbinu bora za kutatua changamoto hizo lakini pia kuimarisha ubora wa elimu nchini.
Amesema kupitia mkutano huo mafanikio mbalimbali yamepatikana ikiwemo kujengwa kwa ofisi za elimu kila Wilaya pamoja na kuanzishwa program ya skuli connecting ambayo inaziunganisha skuli mbali mbali katika kufunza na kufundishia.
Akizungumza kwa niaba ya Asasi za kiraia zinazofanya kazi Zanzibar chini ya mtandao wa elimu Zanzibar Bwana KAISAR MOHAMMED SAID amesema asasi za kiraia zimekuwa nguzo muhimu katika kuwajengea elimu watoto wa kizanzibari na kuleta mabadiliko ya kweli kupitia program bunifu na mbinu mbalimbali za kujifunzia bila ya kuwasahau wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
KaAISAR amefahamisha kuwa msingi wa elimu bora kwa wanafunzi unaanzia kwa kuwa na mashirikiano ya karibu kati ya wazazi, walimu, kamati za skuli na wizara ya elimu ambayo yatatoa matokeo chanya katika kuimarisha sekta ya elimu nchini.
Amesema Asasi za Kiraia kwa kushirikiana na serikali na wadau wa elimu watahakikisha watoto wote wanapata fursa sawa za elimu na kuwajenga kuwa bora na wenye kukabiliana na changamoto zinapojitokeza.
Imetolewa na Kitengo cha Habari WEMA