
Leo tarehe 2 Januari 2026, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Ndg. Khamis Abdulla Said, akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndg. Amos John Henock, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ndg. Mohamed Ali Abdalla, wamefanya kikao na wananchi wa Kiembe Samaki katika Skuli ya Msingi Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi, kujadili eneo lilipo katika skuli hiyo linalotarajiwa kufanyiwa ujenzi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zinazojitokeza kufuatia ujenzi huo.