
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesisitiza dhamira yake ya kuendeleza kuimarisha ushirikiano wa kielimu na India, ikitambua mchango mkubwa wa nchi hiyo katika kuinua viwango vya elimu na kutoa nafasi za mafunzo kwa wanafunzi na wataalamu wa Zanzibar.
Akizungumza katika ukumbi wa mkutano wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali huko Mazizini, Mheshmiwa Lela Muhamed Mussa ameishukuru kwa dhati Serikali ya India kwa kuendelea kusaidia sekta ya elimu kupitia programu, ruzuku na ubadilishanaji wa wataalamu.
Aidha, ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya India kwa ushirikiano wao katika elimu kwani kuna mengi ya kujifunza kutoka kwao na kuhakikishia kwamba milango iko wazi, na mawaziri wako tayari kushirikiana katika masuala haya.
Nae Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali bi Khadija Salum Ali amehimiza kudumisha ushirikiano na kusema Zanzibar ipo tayari kupokea Walimu kutoka India kwani mpango huo utaongeza uzoefu kwa wanafunzi wa Zanzibar.
Pia Balozi wa India Nchini Zanzibar Mheshmiwa Bishwadip Dey, amesema kuna Programu mbili kuu za elimu ambazo zinashirikisha India na Tanzania: moja ni programu ya ITEC, ambayo inatoa mafunzo yasiyolipishwa kwa kipindi cha wiki mbili hadi mwaka mzima. Pia, progrqmu ya bodi ya elimu ya kimataifa ambapo wanatoa scholarships za masomo kwa kiwango cha bachelor, master, na PhD.

Nae Mkurugenzi aliyemaliza muda wake katika Taasisi ya Indian Institute of Technology Madras Prof. Preety ameioingeza Wizara ya Elimu kwa jitihada inayoichukua katika kunynanyua Sekta ya Elimu ikiwemo kuanzishwa kwa Chuo hicho Chenye ya Kimataifa na ameahidi kuendelea kuipatia Serikali mashirikiano kwa lengo la kuifanya Zanzibar kua chemchem ya Kitaaluma hali ambayo itachochea wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali kusoma Zanzibar.
Zanzibar inajivunia kuwa na mahusiano na India, na inatarajia kua na ushirikiano endelevu kwa lengo la kuketa mabadiliko chanya katika jamii.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na uhusiano – WEMA