
Uongozi wa Idara ya Elimu Mbadala na Watu wazima Ukiongozwa na Mkurugenzi wa Idara hiyo Ndg. Mashavu Ahmada Fakih umekutana na kufanya kikao na Ujumbe kutokaTume ya taifa ya UNESCO kutoka Jamuhuri ya Korea na Tume ya Taifa ya UNESCO Tanzania. Kikao ambacho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano Wizara ya Elimu Mazizini Zanzibar.
Kikao hicho cha siku moja kimefanyika kufuatia ziara za tume hizo kutembelea vituo vya kufundisha kisomo cha watu wazima kupitia Mradi wa “The BridgeTanzania project ” katika Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Mradi wa “The bridge Tanzania project” umeanzishwa mapema mwaka 2025 kwa lengo la kuwasaidia vijana waliopo kando ya mji kufundisha kisomo kidigitali , ujuzi na ujasiriamali ili waweze kusoma na kuandika na kuwajengea uwezo wa kujiajiri, Mradi huo kwa sasa umeanza katika Wilaya tatu amabazo ni Geita na Masasi kwa Tanzania bara na Kaskazini A kwa upande wa Zanzibar.

“The bridge Tanzania project” unafadhiliwa na Tume ya Taifa ya UNESCO kutoka Jamuhuri ya Korea kwa kushirikiana na Idara ya Elimu Mbadala na Watu Wazima Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Tanzania bara.
Imetolewa na kitengo cha Habari na Uhusiano, WEMA – Zanzibar.