
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mheshimiwa Lela Muhamed Mussa amewataka Wafanyakazi wa WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuiendeleza tunu ya upekee waliyonayo ya umoja, upendo na mashirikiano.
Akizungumza katika hafla ya kuwakaribisha na kuwaaga baadhi ya viongozi hapo Mazizini kwenye Wizara ya elimu, Mheshimiwa Lela amewataka wafanyakazi kujua ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyoelekeza katika sekta ya elimu ili kufikia lengo lililokusudiwa.
AIDHA Mheshimiwa Lela amesisitiza UTEKELEZAJI wa mpango wa Elimu wa WIZARA ili kutimiza jukumu la Elimu kwa wananchi wa Zanzibar na kutimiza maono ya viongozi wetu.
Katika hafla hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ndugu Khamis Abdulla Said katika taarifa yake ya kiutendaji na Muundo wa WIZARA amesema kuwa jumla ya miradi mikuu mitatu inasimamiwa na Wizara hiyo.
Akiwaga wafanyakazi wa WIZARA aliyekuwa Naibu waziri wa Elimu Mheshimiwa Ali Abdul-ghulam Hussein ametoa shukrani zake kwa wafanyakazi kwa kuonyesha umahiri wao wakati wote wa uwepo wake.
Nae Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mheshimiwa Khadija Salum Ali amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziI Dr. Hussein Ali Mwinyi kwa kumuamini kwa kumpa jukumu katika Wizara ya Elimu na ameahidi kufanyakazi kwa bidi na mashirikiano ili kuacha alama katika Wizara ya Elimu.
AIDHA amewataka wafanyakazi hao kuonyesha mashirikiano zaidi ili kuendeleza mbele maendeleo ya Elimu.
Nae Naibu katibu Mkuu Taaluma Dr. Mwanakhamis Adam Ameir amemuhakikishia Mheshimiwa Waziri kuwa wafanyakazi wapo tayari kufanyakazi kwa Kasi kubwa ili kuendeleza mbele maendeleo ya Wizara.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Ina jumla ya Wafanyakazi 20,566 idadi AMBAYO imejumuiaha Idara, Vitengo na Taasisi za Unguja na Pemba.
Imetolewa na kitengo Cha habari, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.
Tarehe 24/11/2025