Serikali imetowa wito kwa jamii hususan vijana kuweka uzalendo mbele katika matumizi ya teknolojia kwa maendeleo ya taifa letu na vizazi vinavyokuja. Wito huo umetolewa na Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Mahamoud Thabit Kombo kwa njia ya mtandao wakati wa kufunga mafunzo ya siku kumi ya kuimarisha umahiri wa TEHAMA, hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Nkrumah kiliopo Mfenesini, Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Aidha Dkt. Kombo amesema; “Leo ni siku ya heshima kuu kwangu kushiriki nanyi katika kufunga rasmi programu muhimu ya maendeleo ya kitaaluma katika Chuo cha Mafunzo ya Ualimu. Tangu tarehe 10 hadi 21 Novemba 2025, walimu 35 wa sekondari na maafisa wa TEHAMA wamepata mafunzo makubwa na ya kubadilisha mtazamo, wakiboresha ujuzi wao na uwezo wa kulitumikia taifa letu.
Ninatoa shukrani za dhati kwa washirika wetu wote waliowezesha kufanyika kwa programu hii. Tulianza safari hii nilipokuwa Balozi.