
Naibu Katibu Mkuu Utawala Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndg. Khalid Masoud Waziri leo tarehe 10/11/2025 amepokea ujumbe kutoka Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA) uliofika ofisini kwake Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na kufanya mazungumzo kuhusu namna bora ya kukuza mashirikiano baina ya Japani na Zanzibar katika Maendeleo ya sekta ya Elimu.