
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (WEMA) imeishukuru Taasisi ya Good People kwa ushirikiano wanaoutoa ili kuhakikisha Watoto wanajifunza katika mazingra mazuri.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Maandalizi na Msingi Bi Fatma Mode Ramadhan, ameeleza hayo katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa uboreshaji wa Mazingira ya Elimu uliohusisha ujenzi wa Madarasa katika Skuli ya Msingi ya Jumbi pamoja na Ndijani, Mkoa wa Kusini Unguja.
Aidha amesema, Mradi huo ni zawadi kwa Serikali ambao itasaidia Walimu kufikia utekelezaji wa Mtaala kwa ufanisi kwa kuwapatia muda rafiki wa kufundisha kupitia mkondo mmoja.
Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Good People Bi Mi sook, Choi ameishukuru Serikali kwa kutoa ruhusa ya kuanzisha mradi huo wa ujenzi na kuiomba jamii na Taasisi nyengine kuiga mfano huu kwani Elimu ni ufunguo wa maisha.
Nae mwalimu wa Skuli ya Msingi ya Jumbi bi Warda Suleiman Ali amesema, kukamilika kwa mradi huo kutapunguza mrundikano wa idadi kubwa ya Wanafunzi madarasani na kuweza kupata wepesi katika ufundishaji na kuongeza ufanisi.
Mradi huo uliodhaminiwa na Taasisi ya Good People iliyo jitolea kujenga jumla ya Madarasa 10, ambayo 7 kwa upande wa Jumbi na 3 Ndijani.
Imetolewa na Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano, WEMA.