
Mkoa wa mjini magharib.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imewataka wahudumu wa skuli za maandalizi kua na subra na kufanya uadilifu katika kutekeleza majukumu yao ya kazi ya uhudumu kwa wanafunzi.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Maandalizi na Msingi Bi Fatma Mode Ramadhan wakati akizungumza na wahudumu wa skuli za maandalizi, leo TAREHE 3Novemba 2025, Mkoa wa Mjini Magharib katika ukumbi wa kariakoo. Ambapo amewasisitiza wahudumu hao kua na heshima na nidhamu na kuwajibika katika majukumu yao.
Aidha Mkurugenzi Fatma amewatataka wahudumu hao kudumisha usafi, kuzingatia usalama wa watoto, kupika chakula katika mazingira mazuri, pamoja na kuepuka dharura zisizo na msingi, na kuwa wakarimu kwa wanafunzi wote wakiwemo wenye mahitaji maalumu ili kuwajenga wanafunzi katika masomo yao.
Nae Mkuu wa Divisheni ya Maandalizi Mwalimu Hamad amemshukuru Mkurugenzi wa Idara hiyo kwa kupigania kupatiwa wahudumu wa skuli za maandalizi ili kupunguza majukumu kwa walimu na kuwafanya watimize mtaala kwa ufanisi.
Nao wahudumu hao wameahidi kushirikiana kikamilifu na walimu ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu katika mazingira mazuri na kutoa wito kwa jamii waendelee kujitolea ili kuimarisha maendeleo.
Wahudumu hao wameajiriwa chini ya kampuni ya Broad Way iliyo chini ya Mwenyekiti Bwana Haji Yussuf Abdallah.
Imetolewa na Kitengo cha Habari, Mawsiliano na Uhusiano WEMA.