THE Revolutionary Government of Zanzibar

Ministry of Education and Vocational Training

UZINDUZI WA MUONGOZO WA LISHE KATIKA SKULI

Mkuu wa Kitengo cha Elimu Mjumuisho na Stadi za Maisha Ndg. Juma Salim Ali amesema Muongozo wa lishe katika skuli umekuja kutoa maelekezo juu ya namna ya kuwapatia chakula bora wanafunzi ili wawe na afya bora na kuweza kufanya vizuri katika masomo yao.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Idara ya Elimu Maandalizi na Msingi Bi Fatma Mode Ramadhan amesema muongozo huo umekuja baada ya kufanya tafiti mbali mbali kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na kubaini kuwa wanafunzi walio wengi wana tatizo la upungufu wa damu hasa watoto wa kike.

Aidha ameeleza kuwa hatua hiyo pia imetoa maelekezo ya kupatiwa elimu na miongozo kwa wauzaji wa chakula skulini kuuza chakula bora na chenye Afya kwa wanafunzi ili lengo liweze kufikiwa.

Nae Afisa Msingi juu Idara ya Elimu Maandalizi na Msingi Ndg. Ali Makame Haji amesema muongozo huo utasaidia kupunguza tatizo la uzito uliokithiri au unene uliopitiliza pamoja na kutatua tatizo la utapia mlo unaosababishwa na ukosefu wa virutubisho kunakotokana na kutozingatia uwiano wa mlo kamili.

Imetolewa na Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano WEMA.