
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziI Dr. Hussein Ali Mwinyi amewaahidi walimu kuwa serikali itazidi kuzifanyia kazi changamoto zote zilizoainishwa katika MAADHIMISHO ya walimu DUNIANI.
Akizungumzia huko viwanja vya Ziwani, Polisi Rais Mwinyi amesema serikali yake Kila mwaka itaajiri walimu kutokana na mahitaji.
Aidha Dr. Mwinyi ametia maagizo kwa UONGOZI WA WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuhakikisha kuwa inaandaa utaratibu utakao hakikisha madai yote ya walimu yanatekelezwa.
Kwa upande wa sekta ya Elimu kwa ujumla Rais Mwinyi ameahidi kuipa elimu kipaumbele Cha hali ya juu zaidi endapo serikali yake itarejea tena madarakani.
Aidha amewataka wananchi kuimarishwa amani na utulivu wakati wote wa uchaguzi na baadae ya uchaguzi.

Akimkaribisha mgeni rasmi, Rais wa chama Cha walimu Zanzibar ndugu Seif Mohammed Seif amesema walimu wa Zanzibar tayari wameshajitambua kutokana na utekeleza wake na kuwajali walimu.
Akisoma risala ya walimu Katibu Mkuu wa chama Cha walimu ZATU Haji Juma Haji amempongeza Dr. Husseini Ali Mwinyi kwa kuwajali walimu na kutimiza Yale yote aliyowaahidi walimu katika kipindi Cha miaka mitano, ikiwemo kuimarishwa kwa Miundo mbinu ya skuli, kuongeza idadi ya walimu, kuongeza idadi ya mikopo ya Elimu ya juu na maslahi ya walimu ikiwemo mishahara na posho.
Akitoa salamu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Katibu Mkuu ndugu Khamis Abdulla Said amesema mwalimu ni zaidi ya mfanyakazi wa kawaida kwa kuwa yeye ndie humvusha mtoto kutoka katika hali ya ujinga na kumpeleka katika ngazi ya ufahami.
Aidha ndungu Khamis amesema siku ya walimu ni siku ya kujitafakari kwa kazi kubwa inayofanywa na walimu na kumshukuri Mheshimiwa Rais wa Zanzibar kwa kuwajali walimu na Wizara kwa ujumla.

Nae Katibu Mkuu wa ZATUC Khamis Mwinyi Mohammed akitoa salamu za ZATUC amemsifu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziI Dr. Hussein Ali Mwinyi kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kuipa kipau mbele sekta ya Elimu ndani ya miaka mitano na kukirejesha Chuo Cha ualimu Nkrumah.