
Leo tarehe 12/09/2025 Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Mhe.Amour Yussuf Mmamga amemkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdullah Said eneo la ujenzi wa skuli ya msingi huko Shangani.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo Katibu Mkuu ameushauri uingozi wa wilaya hiyo kutenga maeneo kwa ajili ya Ujenzi wa skuli na kuwataka tume ya mipango kufanya tathmini ya mazao yaliyomo katika eneo hilo kwa ajili ya kulipa fidia.
Amesema hatua hiyo ni kwa manufaa ya watoto kuepukana na changamoto mbali mbali ikiwemo kufuata skuli masafa marefu.