
Katibu Mkuu wa Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdullah Said leo tarehe 12.09.2025 amekagua eneo la ujenzi wa kituo cha ubunifu wa tehama, ambapo eneo hilo limevamiwa na wananchi na kuendeleza shughuli za ujenzi huko Bwefum.
Akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali katika ziara hiyo akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano na Uchukuzi Bi Hawwah Ibrahim Mbaye pamoja na Mkuu wa Wilaya wa Magharib B Bwan Amour Yussuf Mmamga amesema nivyema Eneo hilo lipandwe miti kwa ajili ya kuweka alama ya kudumu.
Aidha katibu Khamis amemtaka Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi aombe kibali kutoka Halmashauri kwa ajili ya kuanza utaratibu wa ujenzi wa chuo hicho.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Magharib B Mhe. Amour Yussuf Mmamga amewasisitiza wananchi kufuata taratibu na sheria zilizowekwa kabla ya kuanza ujenzi ili kuepuka usumbufu.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi Bi Hawwaah Ibrahim Mbaye ameombwa kukata kibali kwa Halmashauri kwa ajili ya kuanza taratibu za ujenzi wa chuo hicho