
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa amesema ushirikiano wa baina ya nchi ya Canada na Tanzania katika sekta ya elimu umesaidia kukuza sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kukuza vipaji na uwezo wao kutokana na matumizi ya akili mnemba pamoja na matumizi ya sayansi na technolojia.
ameyasema hayo leo tarehe 22 Julai 2025 katika Skuli ya Sekondari Mwera Pongwe Kisiwani Unguja, katika hafla kuimarisha mfumo wa elimu katika ufundishaji na kupatiwa ujuzi kwa wanafunzi walioshindwa kuendelelea na Elimu ya lazima ili waweze kujiajiri wenyewe kwa maendeleo ya Taifa letu.
Mhe. Lela amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na nchi ya Canada hasa katika kukuza sekta ya Elimu, na ameishukuru Nchi hiyo kwa kusaidia mabadiliko ya elimu Zanzibar
Kwa upande wao Katibu wa Maendeleo ya Kimataifa Nchini Canada Mr. Randeep Sarai na Balozi wa Canada, Tanzania wamepata fursa ya kuangalia fursa za vijana na kazi mbali mbali za amali wanazozifanya kutokana na ujuzi waliopatiwa kupitia mradi wa UNICEF
Wanafunzi hao wa Skuli ya Sekondari Mwera Pongwe wamekua wanufaika wakubwa kutokana na ushirikiano wa Canada na UNICEF katika kuimarisha Afya na Taaluma za wanafunzi pamoja na kuongeza kiwango cha ufaulu katika Elimu.
Kupitia mpango wa afya na lishe wa skuli za Zanzibar unaotekelezwa na UNICEF zaidi ya wanafuzi wa kike 38,000 wamepatiwa virutubisho vya Iron na Folic acid kila wiki na vijana 72, 000 wamenufaika na elimu ya lishe bora ili kuimarisha afya zao na kukuwa kitaaluma.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSINAO (WEMA)