
Leo tarehe 15/07/2025, Naibu katibu Utawala Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (WEMA) Ndg Khalid Masoud Wazir na Naibu katibu taaluma Dkt. Mwanakhamis Adam Ameir wamekutana na ujumbe kutoka Shangai-China uliolenga kuimarisha uhusiano na kuwajengea uwezo waalimu wa masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM).
Akizungumza na ujumbe huo huko katika ofisi za WEMA Mazizini Naibu katibu Khalid amesema Wizara inashirikiana na wadau mbali mbali ili kuhakikisha kiwango cha Elimu Zanzibar kinaimarika hasa katika masomo hayo.
Amefahamisha kuwa lengo kuu la ushirikiano na Shangai ni kuimarisha mipango mkakati ya ufundishaji kwa somo la hisabati ili wanafunzi walipende somo hilo na kukuza kiwango cha ufaulu.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA).