Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa akiambatana na viongozi mbali mbali wa Wizara hiyo wamepokea ugeni wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania Nathan Balete katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Elimu Mazizini – Unguja.

Mkurugenzi wa Benki ya Dunia alipata fursa ya kupokea ripoti ya utekelezaji wa mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya msingi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia iliyowasilishwa na katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ndugu. Khamis Abdullah Said.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusino WEMA
16/06/ 2025