Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amli Zanzibar (WEMA) Ndg. Khamis Abdalla Said amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Mashirika ya Maendeleo na Asasi za Kiraia katika kuimarisha sekta ya Elimu nchini.
Ameeleza hayo wakati akifunga Mkutano wa Nane (8) wa Wadau wa Kutathmini Maendeleo ya Sekta ya Elimu Zanzibar huko Mbweni, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Katibu khamis amefahamisha kuwa Mashirika na Taasisi hizo zimekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio yaliyofikiwa sasa katika sekta ya elimu nchini.
Amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta ya elimu katika maendeleo ya taifa imewekeza zaidi ili kuhakikisha kunakuwa na wataalamu wa kada mbali mbali, ambapo madarasa 20 ya smart yanatarajiwa kujengwa ili kurahisisha upatikanaji wa elimu na kutatua tatizo la uhaba wa waalimu uliopo hasa katika masomo ya sayansi na hisabati.
Nao Washirika wa maendeleo nchini wamesema wataendele kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu Zanzibar.