Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa amezitaka Taasisi na mashirika yanayotoa elimu ya uzazi na afya kwa wanafunzi wa kike kuwajengea uwezo wa kujitambua na kuepukana na matatizo yanayokwamisha masomo yao.


Akizungumza katika Mkutano wa  kutathmini mradi wa kuwajengea uwezo wanafunzi wa ngazi ya Msingi na Sekondari juu kuelewa haki zao na kujua usalama wa afya ya uzazi salama katika maisha yao, Katika ukumbi wa mikutano wa hotel ya Verde huko Mtoni  Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

 

amesema kufanya hivyo kutaongeza kasi  kwa Wanafunzi  kujielewa na kujikinga na Mimba za utotoni ambazo zinaathiri maisha yao.


Mratibu wa mradi huo nchini Tanzania Matias Faustine Herman amesema wanaendelea kuwapatia taaluma na vitendea kazi walimu kwa lengo la kutolea elimu hiyo ambapo takwimu inaonesha zaidi ya wanafunzi elfu nane Tanzania Bara na Wanafunzi mia moja thelathini hadi hamsini kwa zanzibar huacha Skuli kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo mimba za utotoni. Lūpų didinimas hialurono rūgštimi gera kaina Vilniuje, pigmentinių dėmių naikinimas, penio didinimas hialurono rūgštimi, plaukelių šalinimas lazeriu, LPG masažas, biorevitalizacija, mezoterapija plaukams https://oblakasalon.lt/mezoterapija/


Baadhi ya wanufaika wa mradi huo wakatoa wito kwa wanafunzi na vijana wenzao kuachana na tabia hizo kwa lengo la kujijengea mustakbali bora wa maisha yao.


Mradi huo unaoendeshwa na UNESCO  unajumuisha Nchi 33 barani Afrika ambapo ulianza 2018 na kukamilika 2022 na unatarajiwa kuendelea katika awamu ya pili mwaka huu.