Idara ya TEHAMA katika Elimu inawatangazia walimu wote wenye sifa kuomba kujiunga na mafunzo ya elimu, ubunifu na TEHAMA kwa njia ya mtandao. mafunzo hayo ya awamu ya pili yanatolewa kwa miezi tisa (9) kuanzia mwakani 2024, kwa ushirikiano wa kampuni inayotengeneza vifaa vya TEHAMA ya HP kupitia programu yao ya HP IDEA (Innovation and Digital Education Academy). sifa za waombaji ni kama ifuatavyo:-

  1. Walimu wawe ni waajiriwa wa skuli za serikali na idadi ya walimu iwe kuanzia walimu watatu kwa kila skuli.
  2. Walimu wawe na uwezo wa kutumia na kupata kompyuta, simu janja au kishkwambi, Pamoja na internet iwe kutoka Skuli yake, vituo vya ubunifu wa kisayansi (hubs) au vituo vya ualimu (TCs) au intaneti ya simu yake.
  3. Aweze kutenga muda wa masaa mawili kila siku ya Jumatano saa nane hadi saa kumi jioni kwa kuingia katika darasa.
  4. Aweze kutenga muda wa mafunzo ya vitendo na ushirikiano angalau masaa sita kwa wiki.
  5. Mwalimu awe na barua pepe yake (email address) na whatsapp.
  6. Mwalimu aweze kusikia na kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha.

Waombaji watume barua zao za maombi pamoja taarifa binafsi (CV) zao kupitia email zifuatayo:- This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.  nakala itumwe kwa This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 20.12.2023.

TANBIHI:

Mafunzo haya hayatakuwa na malipo ya posho au nauli.