Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bi Asya Iddi Issa amesema kupewa Mafunzo ya kuisimamia na kutunza kumbukumbu ya matumuzi ya fedha kutawasaidi kutimiza majukumu yao.


Hayo ameyasema wakati wa kufungua Mafunzo kwa Walimu Wakuu na washika fedha wa Skuli za Sekondari Unguja Katika ukumbi wa mikutano Skuli ya Dk Ali Mohamed Shein Wilaya ya Mjini Unguja.


Amesema Mafunzo hayo kwa Walimu kutawasaidia  kuweza kupanga utaratibu mzur wa matumuzi ya fedha kwa kila mwaka.


Pia aliwasisitiza washika fedha hao kuhakikisha  wanatunza risiti za matumuzi katika Skuli zao kwani ndio njia itakayoonesha matumizi ya fedha za Serikali.

Bi Asya amewasisitiza kuhakikisha wanapitia ripoti ya Mkaguzi wa hesabu wa wizara na kuyafanyia kazi mapungufu yatakayojitokeza.

 


Mapema akiwasilisha hoja zilizojitokeza katika ukaguzi wa Skuli za Unguja na Pemba Mkaguzi wa hesabu za ndani Wizara ya Elimu Zanzibar bwana jabir Kipenda jabir  amesema Walimu Wakuu anawajibu wa kuhakikisha matumizi yote yanayofanyika katika Skuli yake anayajua kwa kuwa na ithibati ya uingiaji wake na utokaji wake.


Aidha amewataka kuhakikisha wanapotaka vifaa wafate utaratibu wa kuandika barua ili kupata uhalali wa watumizi wa vifaa bila ya kuleta mashaka.


Mafunzo hayo ya siku moja yamewashirikisha Walimu Wakuu na washika fedha wa Skuli za Sekondari Unguja.