Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgulam Hussein amesema Serikali ya Awamu ya Nane chini ya uongozi wa Mhe Dkt Hussein Ali Mwinyi inatumia kila jitihada kuekeza katika sekta ya Elimu ili kuzalisha vijana wenye katika fani  mbalimbali.


Amesema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Wanafunzi waliopata nafasi za masomo nchini Ras el khema katika ukumbi wa mikutano Mazizini Unguja.


Amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu  inatumia fursa mbalimbali kwa kuhakikisha Wanafunzi wanasoma kwa kutumia mikopo na ufadhili mbalimbali ili taifa lizalishe wataalam wazalendo.


Amesema ni imani ya Wizara kwa Wanafunzi waliopata daraja la awali watapata ufadhili wa masomo hasa masomo ya sayansi kutokana na kuwepo kwa fursa mbalimbali.


Akiwapa nasaha Wanafunzi hao amewasisitiza kudumisha Nidhamu, heshima na Mila za Taifa lao kwani hiyo ni njia moja wapo ya kutangaza  mambo mema ya Taifa lao.


Aidha amewata kuhakikisha wanadumisha  mashirikiano na Wanafunzi wenzao ili waweze kutimiza ndoto zao na kuweza kurudi na matokeo mazuri.


Pia amewata wazazi itakapo tokaea changamoto yeyote kwa watoto wao wawe mstari wa mbele kushirikiana na bodi ya mikopo Zanzibar kwa kulitatua na sio kusambaza changamoto hizo bila ya kushirikiana na sehemu husika.

 

Nae Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Khamis Abdulla Said amesema Serikali ya awamu ya nane itaendelea kuhakikisha inaboresha sekta ya Elimu ili kufikia Dira ya maendeleo ya 2050 ya Zanzibar kufikia uchumi wa kati.


Amesema Wizara itaendelea kufanya bidii ya kutoa mikopo na kutafuta ufadhili wa masomo ili kuhakikisha Zanzibar inakua na wataalam wazalendo.


Mapema Mkurugenzi Bodi ya Mikopo Zanzibar ndugu Iddi Khamis Haji amesema  ni utaratibu unaofanyika kila mwaka kupata nafasi za masomo kutoka lkatika mfuko wa hifadhi ya Ras el khema  zinazotolewa na Taasisi ya Kassim Foundation.


Amesema kwa mwaka huu ni vijana watano waliopata fursa hiyo kutokana na ufaulu wa daraja la awali kutoka ufaulu wa  sayansi katika tahasusi PCM.


Akitoa neno la shukrani mmoja wa wazazi wa Wanafunzi hao amesema watahakikisha wanashirikiana na Wizara  ili kuona watoto wanapata Elimu itakayonufaisha Taifa lao.


Wanafunzi hao watano  ni kundi la Saba ambapo limeingia Katika ufadhili wa  masomo nchini Ras El Hema.