Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhammed Mussa amesema, Wizara Inathamini jitihada za Wadau mbali mbali katika Sekta ya Elimu ili kuleta maendeleo mazuri ya Elimu Zanzibar.
Ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Dahali ya Kisasa ya Wanawake iliyo jengwa na Tasisi ya korea Food for the Hungry International (KFHI ) chini ya Ufadhili wa Ushirika wa Maendeleo Korea International Coperation Agency iliyoko huko Paje Mtule Wilaya ya Kusini Unguja.
Amesema, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Zanzibar imekuwa ikipokea misaada mbali mbali kutoka Kwa wadau mbali mbali ili kuweza kuboresha maendeleo ya Elimu Zanzibar.
Amesema, Wizara itaendelea kutoa mashirikiano na Wadau wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu ili kuweza kudumisha umoja na mashirikiano katika kuiboresha Sekta ya Elimu pamoja na sekta nyengine zote za kimaendeleo.
Aidha Waziri Lela, amesema Serikali ya Awamu ya nane chini ya Ungozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinfuzi Dkt Hussein Ali Mwinyi kipao mbele chake ni Elimu hivyo Wizara itahakikisha inatoa Elimu Bora bora ili dhamira ya Serikali iweze kufikiwa lengo.
Aidha, Waziri Lela amewataka Wanafunzi kuitunza dahalia hiyo ili iweze kutumika kwa muda pamoja na kuongeza jitihada ili wafaulu vizuri mitihani yao.
Aidha amewashukuru wafadhili hao kwa kuunga mkono Sekta ya Elimu Zanzibar na kuahidi kuzithamini juhudi hizo ili kuleta mafanikio ya Elimu Nchini.
Mapema, Mkurugenzi Mtendaji wa KOICA nchini Tanzania Mr Mansik Shin amesema wamedhamiria kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wa kike kwa. Lengo la kuwajea Mustakbali mzur wa maisha yao baadae.
Nae Mkurugenz Mtendaji wa Tasisi ya Wanawake Initiative foundation (MIF )Bi Sabra Muhammed amesema Tasisi imekabidhi Magodoro 1881, Sukari Tani Tano na Robo, Unga , Mchele na Mafuta kwa skuli zote 35 zilizopo Mkoa wa Kusini Unguja kwa ajili ya kusaidia Wanafunzi wa Kidato cha Nne ambao ambao wapo Kambini. PVC täispuhutavad kummipaadid hea hinnaga siin
Amesema ni Mwaka Mmoja Tangu ianzishwe Tasisi ya Mwanamke Initiative Foundation lengo lake ni Kukuza Ufaulu na kutokomeza Sifuri kwa Wanafunzi katika Mkoa wa kusini Unguja.
Amesema, katika kuhakikisha Ufaulu unaengezeka kwa Mkoa wa Kusini Unguja Tasisi hiyo inakusudia kufanya juhudi mbali mbali ikiwemo kuwapatia Mafunzo Maalum Walimu wote na Wanafunzi pamoja na vifaa vitakavyo wasaidia pindi wanapo durusu masomo yao.