Kufanya kazi kwa bidii katika utowaji wa Taaluma kutasaidi kuleta Mabadiliko na Maendeleo yaliyo bora kwa Taifa.

Amesema hayo katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw. Khamis Abdulla Said, wakati akifunga mafunzo ya Siku mbili yaliyo andaliwa kwa mashirikiano ya Idara ya Elimu Mbadala na Tume ya Taifa UNESCO kutoka Jamuhuri ya Muungano Tanzania. iliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Unguja.

Amesema, kuna baadhi ya Wakufunzi hawawajibiki ipasavyo jambo ambalo hupelekea kurudisha nyuma maendeleo ya elimu nchini.

Aidha, amewataka Wakufunzi hao waliopatiwa mafunzo kuyatumia ipasavyo kwa kuwapa vijana ujuzi uliobora utakao weza kuwasaidia katika Maisha yao ya Baadae.

 Aidha, Bw. said amelishukuru shirika la Taifa (UNESCO) kwa kuandaa Mradi huo na kuuwasilisha kwa lengo la kutaka kuwaengezea ujuzi Wakufunzi wa Idara ya Elimu Mbadala.

Mapema Mkurugenzi Idara ya Elimu Mbadala na Watu Wazima Bi. Mashavu Ahmada Fakih, amesema, kutolewa kwa Mafunzo hayo Idara inaamini yatakwenda kujenga utendaji kazi kwa ufanisi zaidi.

Amesema, kutokana na Mazingira ya kituo cha Elimu Mbadala na fani zinazotolewa basi mafunzo hayo yatasidia na kupunguza changamoto zilizo kuwepo katika swala zima la utowaji wa taaluma kwa vijana.


Nae Naibu katibu Tume ya Taifa UNESCO Tanzania Bw. Aboud Khamis amesema, Mafunzo hayo yamefanyika kutokana na utekelezaji wa programu shirikishi ambayo inafadhiliwa na Shirika la Utamaduni,  Sayansi la  Umoja wa Kimataifa(UNESCO ) lengo lake ni kuwajengea uwezo Walimu wavituo vya Elimu Mbadala ili waweze kupata Marifa Mapya na Stadi zilizo bora wakati wa ufundishaji.


Kwa upande wao Washiriki wa Mafunzo hayo wameushukuru uongozi wa Idara ya Elimu Mbadala pamoja na Tume ya Taifa UNESCO kwa kuwapatia mafunzo hayo  ya uboreshaji katika ufundishaji.

Aidha, wameahidi kuyatumia vyema vyema Mafunzo hayo ili lengo la kuwapatia  wanafunzi fursa za kujiajiri au kuajiriwa liweze kufikiwa.


Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA).
Tarehe: 26/07/2023