Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bwana Khamis Abdulla Said  amesema Wizara ya Elimu ndio yenye dhamana ya kuhakikisha inaandaa vijana wa Taifa lao. Ameyasema hayo wakati alipokutana na watendaji wa Wizara hiyo huko Mazizini  Unguja.                 

Amesema Elimu ndio suala la Msingi katika Maendeleo ya kila Taifa,hivyo ni wajibu wa kila mtendaji kuhakikisha anafanya kazi kwa bidii na maarifa ili Taifa lizalishe wataalamu wazalendo.                        

Amesema Serikali itahakikisha kwamba kila mwananchi anapata fursa ya Elimu .

Akizungumzia  suala la miundombinu  ya Elimu,amesema atahakikisha kuwa kila mtu anahusika ili malengo hayo yafanikiwe.

Aidha akizungumzia mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia amesema ni muda sasa wa Wizara kuendesha mambo kupitia Teknolojia.

Amesema kutokana na mabadiliko hayo ni vyema  kwenda nayo sambamba ili kuhakikisha wanatimiza malengo ya Serikali.

Mapema Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Elimu Zanzibar bi Mtumwa Iddi Hamad amesema wakuu wa vitendo wasimamie watendaji wote ili waweze kufikia malengo ya Serikali.

Pia amewataka watendaji nao kuhakikisha wanatimiza majukumu yao.