Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgulam Hussein  amesema kuwaandaa Wanafunzi kimasomo  kutapelekea kuzalisha wataalamu wenye ufanisi katika fani mbalimbali nchini.

Amesema hayo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo  ya hatua ya kwanza ya kuwaandaa Wanafunzi wa  afya  huko  Zanzibar school of health ZSH Kwa Mchina Mwanzo  Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Amesema kumuandaa  Mwanafunzi  mapema kimasomo ni kumjengea mustakabali mwema katika maisha yake ya Chuo Kwa kipindi chote Cha masomo.

Aidha Mhe Gulam amesema, Wizara ya Elimu kupitia Bodi ya Mikopo iko mbioni kurekebisha Sheria za mkopo ili na wanafunzi wa diploma na waweze kunufaika na mikopo hiyo. Amesema hatua hiyo itasaidia vijana wengi nao kuweza kutumia fursa za masomo.

Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Zanzibar school of health ZSH bi Aziza Hamed amesema, Lengo la Mafunzo hayo ni kuwajenga Wanafunzi kimaarifa na kitaaluma kuweza kupambana na mambo mbalimbali ya Chuo na waweze kutimiza ndoto zao.

Nae mlezi wanafunzi Bwana Suleiman Mahmood Jabir amesema,kuwepo Kwa Mafunzo hayo kutawasadia wanafunzi  kuweza kutatua baadhi ya changamoto na kupelekea kusoma kwa malengo waliojiwekea.

Mafunzo hayo ya wiki Moja yamewashirikisha wanafunzi walioteuliwa kujiunga na Chuo hicho Kwa mwaka wa masomo 2023