Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu na kitekeleza Miradi ya kimkakati  ili kuiwezesha Zanzibar kutumia rasilimali zake ili kufikia malengo ya uchumi wa bluu.

Ameyasema hayo wakati akifungua Mafunzo Maluum ya kuwajengea uwezo maafisa viungo wa Mradi wa Sebep katika suala zima la ujumuishaji wa kijinsia katika ukumbi wa Mikutano Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) Kampasi ya Maruhubi Mkoa wa Mjini Maharibi 

Amesema mradi huo utasaidia Taifa kufikia malengo yake kutokana na mazingira ya nchi. Pia amesema mafanikio ya mradi huo yatafikiwa kwa wakati na ufanisi iwapo utazingatia masuala ya jinsia.

 

Aidha amewataka maafisa hao kuhakikisha wanafatilia mabadiliko ya Maendeleo ya kitaaluma ili kuimarisha mradi huo na vijana waweze kijiajiri na kuajirika.


Nae meneja mradi huo Bwana Salum Mkubwa Abdullah amesema mradi wa sebep utahakikisha kila mtu ananufaika na matokeo ya mradi huo.


Amesema mradi huo ili umfikie kila mtu lazma washiriki wapatiwe mafunzo ili nao waweze kumfikia kila mtu kwa namna yake.


Mradi wa sebep umefadhiliwa  na Benki  ya Maendeleo ya Africa  Kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.