Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Khamis Abdulla Said amesema ili kufikia malengo ya sekta ya Elimu ipo haja ya kuendelea kuwajengewa uwezo watendaji mbalimbali kwanzia viongozi hadi wanaowasimamia.
Amesema hayo wakati wa kufungua Mafunzo ya Uratibu wa wazi wa kupima utendaji kazi wa watumishi katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Utalii Maruhubi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
Amesema kuwepo kwa Mafunzo husaidia kufikia malengo ya taasisi husika kwa wakati. Amewataka washiriki hayo kuitumia vyema fursa hiyo na kuyafata kwa vitendo ili kufikia malengo ya taasisi zao.
Mpema Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji wizara ya Elimu ndugu Mtumwa I. Hamad amesema Mafunzo hayo yatasaidia watendaji kufanya kazi kwa uweledi wa hali ya juu kwenye majukumu yao na kuwaongoza vyema wanaowasimamia.
Kwa upande wake Mkurugenzi kutoka Taasisi ya Afisi ya Raisi Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (PDB) Dkt Josephine Kimaro amesema katika sekta ya Elimu kunavipaombele mbalimbali hivyo ni jambo zuri kuwapa uelewa watendaji wake kwa kuanza na Wakuu wa Idara zote ili kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa wakati.
Mafunzo hayo ya siku mbili umewashirikisha wakuu wa Idara na wakuu wa vitengo kutoka Wizara ya Elimu Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi ya Afisi ya Raisi Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (Presidential Delivery Bureau PDB).