Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dk. Mwanakhamis Adam Ameir amewataka Wadau wa Elimu kuiga mfano wa KOICA wa Kusaidia na  kuimarisha Maendeleo ya Sekta ya  Elimu Zanzibar ili kuengeza Ufaulu kwa Wanafunzi.

Ameyasema hayo wakati alipofungua kikao cha Tathmini ya nusu Mwaka ya Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari Zanzibar iliyofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip ya Uwanja wa Ndege Mjini Zanzibar.

Amesema KOICA kwa Kushirikiana na Good Neighbers imesaidia sana katika Kuimarisha Maendeleo ya Skuli ikiwemo Kujenga Maabara za Kisasa, Kutoa Mafunzo ya Walimu ya Kuengeza Uwezo wa Kufundishia pamoja na Vifaa na Kuhamasisha Kamati 90 za Skuli za Zanzibar.

Nae Mkurugenzi wa Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu Dk. Suhyun Yoo amesema KOICA itaendelea kushirikiana na Sekta mbali mbali za  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ili Kukuza Miundombinu na  Kuendeleza Kiwango cha Ufaulu wa juu kwa Wanafunzi wa Tanzania_Zanzibar.

Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wamesema wameridhishwa na Maendeleo ya Mradi na Wameushukuru sana Uongozi wa KOICA kwa Jitihada za Kukuza Maendeleo ya  Sekta ya Elimu.

Katika Tathmini hiyo Viongozi mbali mbali wa Wizara ya Elimu ya Tanzania na Zanzibar walihudhuria pamoja na Waakilishi kutoka KOICA na  Good Neighbers na kuweza  Kubadilishana Mawazo.