Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa, leo Tarehe 29/08 /2023, ameshiriki katika Uzinduzi wa Miradi Mbali mbali katika Sekta ya Elimu iliyo zinduliwa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.ikiwa ni Shamra shamra za Kizimkazi Day huko Mkoa wa Kusini Unguja.

Miongoni mwa Miradi iliyozinduliwa ni pamoja na  Ujenzi wa Madarasa Sita katika Skuli ya Msingi Muyuni, Ukumbi wa  Mitihani na Chumba cha Kompyuta  katika Skuli ya  Sekondari Muyuni, Maabara ya Tehama, Elimu Mtandao iliyopo Skuli ya Kizimkazi. 


Miradi hiyo Imefadhiliwa na Wadau mbali mbali wa Maendeleo ya Elimu nchini. wakiwemo PBZ Bank, NMB,  TASAF, na (NGO) ya Mwanamke Intiatives Foundation.


Lengo la kujengwa kwa Miradi hiyo ni Kuinyanyua Sekta ya Elimu nchini ili kwenda sambamba na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia 

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA).