Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Lela Mohammed Mussa amepiga marufuku Vyuo vya hapa nchini kuondoa masomo ya dini na kiarabu katika kutangaza fani zao.
Waziri Lela ameyasema hayo katika uzinduzi wa Maonesho ya Elimu ya Juu uliofanyika katika kiwanja Cha Gombani Chake Chake Pemba.
Amesema imekuaa ni kawaida kwa baadhi ya Vyuo kutangaza fani zao huku wakiainisha Masomo ya Dini na Kiarabu kua hayahitajiki hivyo amevitaka Vyuo hivyo kuacha Mara moja tabia hiyo.
Akifafanua zaidi Waziri Lela amesema tabia hiyo imekua ikiwakatisha tamaa Wanafunzi wa Skuli za Msingi na Sekondari na kuacha kuyasoma Masomo hayo wakiamini kwamba hayahitajiki katika maisha yao.
Amesema Licha ya ukweli kwamba fani zao hazihitaji Masomo hayo hawatakiwi kutangaza kwamba Masomo hayo hayahitajiki.
Akihamasisha Wanafunzi na Wazazi kuitumia vyema fursa ya maonesho hayo amesema Serikali inawekeza nguvu nyingi katika ngazi ya Maandalizi, Msingi na Sekondari hivyo nivyema kuzithamini jitihada hizo kwa kuwaunga Mkono Wanafunzi waweze kujiunga na Elimu ya Juu.
Aidha Mh. Lela ameahidi kuwalipia Wanafunzi Mia moja watakao jiunga na huduma za maktaba katika kipindi hiki Cha maonesho hayo. https://seopaslaugos.com SEO paslaugos ko gero geriausia reklama internete
Nae Mratibu Idara ya Utumishi na Uendeshaji Mwalimu Harithi Bakari Waziri amesema uwepo wa Maonesho hayo utawarahisishia Wanafunzi kuweza kufanya udahili sambamba na kujipatia fursa za Masomo ndani na nje ya Nchi.
Kwa Upande wake Mwakilishi wa Vyuo vinavyoshiriki Maonesho hayo Nd. Issa Mselem Abubakar amesema watajitahidi kutoa miongozo na Ushauri kwa Wanafunzi kabla ya kujiunga na Vyuo.
Jumla ya Vyuo 19 Vimeshiriki katika Maonesho hayo vikiwemo vya Serikali na Vya Binafsi sawa na asilimia 83 ya ongezeko ukilinganisha Vyuo 12 Vilivyoshiriki Maonesho Kama hayo Mwaka Jana.