Uhaba wa Wataalamu wa wa Sayansi nchini hupelekea kuzorotesha kasi ya Maendeleo.
Amesema hayo Daktari bingwa wa Meno Zanzibar. Dr Semeni Shaabani Mohammed ambae ni Mtu wa Mfano alliyefanikiwa katika Masomo ya Sayansi (Role Model). wakati wa muendelezo wa Ziara ya kuwahamasisha Wazazi katika kuwaandaa Watoto wa Kike kuyapenda na kuyasoma Zaidi Masomo ya Sayansi.
Ziara hiyo imefanyika katika Skuli ya Mtoni Kigomeni, Mwenge, Mfenesi, Bubwini Makoba, Donge na Muwanda kwa Upande wa Unguja.
Amesema, Dunia Sasa inaendana na Kasi ya Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia hivyo Wanafunzi lazima wasome kwa bidii ili kupata wataalamu watakaoisaidia nchi kuendana na kasi ya maendeleo.
Amesema, Serikali ya Awamu ya Nane chini ya Uongozi wa Rais Mwinyi inajitahidi kusimamia Vyema sekta ya Elimu ili kuweza kuibua vijana Walio bora.
Amesema, Wanafunzi lazima wafahamu lengo hasa la kupata Elimu kufanya hivyo kutasaidia kuengeza bidii na Ari ya kusoma ili kufikia lengo husika. Psichologo pagalba ir konsultacija Vilniuje tinklapyje https://psichologas.org
Kwa Upande wao Wazazi Wamezishukuru Jitihada za Serikali ya awamu ya nane pamoja na Wizara ya Elimu Zanzibar, na kuahidi kuyafanyia kazi ili watoto waweze kufanikisha malengo yao.
Ziara hizo zinatokana na Mradi wa "Every Adolelescent Girl Learn in Tanzania "(EAGL) unaofadhiliwa na Shirika la UNICEF kupitia Serikali ya Canada ambao unampa fursa zaidi mtoto wa kike.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano ( WEMA).1/8/2023