Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgulam Hussein   amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha sekta ya Elimu inaendelea kupiga hàtua.

Amesema hayo wakati wa hafla ya Ugawaji wa vifaa vya maabara kwa Skuli ya Sekondari Jongowe Wilaya ndogo Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema  Serikali ya awamu ya nane imekusudia kuboresha miundombinu  ya Skuli na upatikanaji wa vifaa vya kufundishia ili taifa lizalishe wataalam wazalendo.

Aidha amesema upatikanaji wa vifaa vya kufundishia vitaleta ufanisi katika kukuza kiwango cha ufaulu nchini.

Mapema akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi Idara ya mipango sera na utafiti wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Khalid Massoud Wazir amewapongeza Shirika la koica kwa kuwa na mikakati  ya kuendelea kushirikiana na wizara ya Elimu Kwa kutoa vifaa, kuwajengea uwezo walimu hasa wa sayansi ili taifa liendelee kukuza ufaulu wa daraja la Elimu.

Mkurugenzi mkaazi wa shirika la Maendeleo kutoka Korea (KOICA) Tanzania bibi jeen amesema shirika  litaendelea kuimarisha mashirikiano mazuri na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuhakikisha wanatoa misaada mbalimbali ikiwemo vifaa vya kujifunzia na kujifunzia,  kuwajengea uwezo Walimu wa masomo ya Sayansi ili  taifa liendelee kukuza ufaulu wa daraja la awali hasa Katika masomo hayo.

Nae  Mwenyekiti wa kamati wa wazazi wa Skuli ya Sekondari Jongowe amesema ni jambo zuri kupatiwa vifaa ila Bado wanauhitaji wa mwalimu wa sayansi ili waweze kulifikia lengo la vifaa walivyo kabidhiwa.

Vifaa mbalimbali vya maabara vilikabidhiwa kwa uongozi wa Skuli ya Sekondari Jongowe Tumbatu.