Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Abdulgulam Hussein amewataka Walimu wakuu kusimamia vyema kamati za shule ili wasaidie kuondoa tatizo la utoro wanafunzi .
Naibu waziri Gulam amesema hayo katika semina elekezi kwa walimu wa kuu wa Skuli za Sekondari za Serikali kisiwani Unguja Katika ukumbi wa mikutano Ocean View huko Kilimani Mjini Unguja.
Amesema ikiwa walimu watatekeleza vyema majukumu yao pamoja na mambo mengine wanakamati watakuwa ni walinzi wa mazingira na miundominu ya skuli.
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema watayatumia vyema mafunzo waliyo patiwa ili kuongeza tija katika maendeleo ya shule zao ikiwemo kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Mafunzo hayo yanayotolewa na taasisi ya good Neighbours yamelenga kuwajengea uwezo walimu wakuu kusimamia vyema kamati za shule zao.