Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa amesema  upatikanaji wa Vifaa vya kujifunzia itasaidia Sana sekta ya Elimu nchini.


Amesema hayo wakati wa hafla ya kukabidhiana Vifaa vya Michezo kutoka Katika Jumuiya ya Zan Education and Sports Initiative (ZESI) Katika viwanja vya wizara ya Elimu Mazizini Unguja.
Amesema upatikanaji wa Vifaa vya michezo hupelekea Wanafunzi kusoma kwa vitendo kitu ambacho kitaleta Ufaulu mzuri nchini.


Aidha amesema Wanafunzi kushiriki Michezo ni jambo litakalo wajenga kiafya na kuwapelekea kuepuka kushiriki katika vikundi  vya  vitendo viovu. 
Pia amewasisitiza Watendaji watakao kabidhiwa vifaa hivyo, kuhakikisha wanavitunza vizuri  vifaa hivyo ili  viweze kusaidia watoto wengi zaidi. 


Aidha ametoa wito kwa Taasisi nyengne kuiga  mfano wa Taasisi ya ZESI . ili kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa kwa wakati.
Akizunguzia suala la Walimu kukataza Wanafunzi kutoshiriki Michezo Waziri Lela amesema, Wizara haitaacha kumchukulia hatua kwani  ni wajibu wake kushuhulikia majukumu mbalimbali yaliopo ndani ya mazingira yake ya kazi.
Mapema kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Khalid Massoud Waziri ameipongeza jumuia ya ZESI kwa kushirikiana na wizara ya Elimu kuhakikisha watoto wanapata Elimu na michezo  kwa kuwa na vifaa vitakavyowawezesha  watoto kucheza kwa umahiri wa hali ya juu.


Nae Muazilishi wa Jumuiya ya ZESI Bwana Ameir Mohammed Makame  amesema Mlengo ya Jumuiya hiyo ni kuendeleza Michezo na Elimu Kwa kufanya Mafunzo mbalimbali yanayohusu Elimu na michezo.
Aidha  amewasisitiza watakaobahatika kupata vifaa hivyo kuhakikisha wanavitumia kutokana na malengo yaliokysudiwa.
Amesema  pia watahakikisha wanatoa vifaa mbalimbali  ikiwemo vya michezo ili kuhakikisha watoto wanaweza kusoma Katika mazingira mazuri na salama.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na mipira ya  mikono, jezi, viti vya kukalia na baskeli.