Naibu Spika wa Wabaraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma amesema, Ushirikiano ni njia moja ya kuleta Mabadiliko ya Kimaendeleo Nchini .

Ameyasema hayo kwa Niaba ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid wakati akifungua Mkuatano wa Wadau wa Elimu  na Kamati ya Ustawi wa Jamii wa Baraza la Wawakilishi Kuhusiana na Utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu wa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET)  uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Chuo cha Maruhubi Unguja

Aidha katika kutekeleza Mradi huo Mhe. Mgeni amehimiza kuwepo kwa Mashirikiano ya karibu kati ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA). Pamoja na Wadau mbali mbali wa Elimu ili kuhakikisha utekelezaji wa Mradi huo unakuwa na Matokeo mazuri kwa Lengo la Kuimarisha Maendeleo ya Elimu kwa Ujumla.

Mapema Naibu Waziri wa Elimu Zanzibar Mhe. Ali Abdulgulam Hussein Amesema, Mradi wa HEET ni Mradi wa Kitaifa ambao unakwenda sambamba na juhudi za Wizara ya Elimu na  Mafunzo ya Amali Zanzibar wenye lengo la kuleta Mageuzi ya Elimu na Kiuchumi.

Amesema, kupitia Mradi wa HEET kiasi cha Dola za Marekani Milioni 7.97,sawa na Wastani wa Shilingi Bilioni 18.23, Ziatatumika kuhusisha kuaanda Mitaala mipya zaid ya 290 ili kuhakikisha Elimu inayotolewa inaenda sambamba na Mahitaji ya Soko la Ajira ndani na Nje ya Nchi. Rachatvotrevoiture.com rachat véhicule accidenté

Amesema, Mradi huo pia Unalenga kusomesha  Wahadhiri 1,100, ambapo Wahadhiri 623 Katika Shahada za Uzamivu (PHD) Wanaume 355 na Wanawake 268. na Wahadhiri 447 katika Shahada ya Umahiri (MSc) Wanawake 197, Wanaume 280. kwa Zanzibar kupitia Chuo Kikuu cha Taifa cha  Zanzibar (SUZA) Wahadhiri 70 watasomeshwa na Mradi huo ili kuweza kuboresha Sekta ya Elimu Nchini.

Nae  Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Professa Mohammed Makame Haji amesema, Kama Tasisi ya Umma ya Elimu ya juu Zanzibar ,( SUZA) inajitolea kutoa Elimu bora ili kuibadilisha Jamii kuwa na Elimu na Taaluma zinazohitajika katika jamii ya Sasa.