Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein, amewataka walimu wa Skuli za Mkoa wa Kusini Unguja kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kujikita zaidi katika kuimarisha elimu kwa wanafunzi ili kutoa matokeo mazuri zaid.

Akizugumza katika mafunzo ya siku nne yaliyoandaliwa na taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation MIF yaliyofanyika katika ukumbi wa TC Dubga Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema, walimu ndio wanaowafanya wanafunzi kuleta  matokeo bora pindi wakitoa elimu inayostahiki kwa wanafunzi wao, hivyo kupatiwa mafunzo hayo itasaidia kujua mbinu za kujibu mitihani kwa wanafunzi na kuengezeka ufaulu kwa wanafunzi wao.

Hivyo, amewaomba walimu kuyatumia mafunzo wanayoyapata na kuyafanyia kazi ili kuimarisha zaid sekta hiyo na kusema bila ya elimu hakutakuwa na tija kwao wala taasi ya elimu.

Sambamba na hayo, Naibu Gulamu, amepongeza jitihada za taasisi za MIF kwani wamekuwa na jitihada za kuona ziro zinaondoka Zanzibar hasa katika mkoa wa kusini.

"Hakika MIF mumekuwa na jitihada za kuona wanafunzi wanafaulu kwa kiwango kikubwa zaidi na hili limeonesha kwenye matokeo ya mwaka huu hivyo muendeleze jitihada hizo" amesema Mhe Gulam. 

Sambamba na hayo, amewataka walimu kuendelea kuweka mazingira bora na imara ili kuweka matokeo zaid kuwa mazuri.

Mapema, Mkurugenzi Mtendaji wa  Mwanamke Initiatives Foundation (MIF), Sabra Ali Mohamed, amesema,  lengo kuu kuwapatia mafunzo walimu hao ni kuona  ufaulu unaengezeka Zanzibar na kusema kuwa mafunzo hayo, yatawasaidia walimu kujua mbinu za kutunga mitihani na jinsi ya kuwafundisha wanafunzi namna ya kujibu mitihani yao ya kidato cha nne.

Hivyo, wameona ni vyema kuwapelekea walimu kutoka Tanzania center of Education, ili kuona wanatoa elimu ya kuona jinsi gani wanauwezo wa kutunga mitihan hiyo na kuona jinsi gani ya kuwapa mbinu ya kujibu mitihani yao na kusema kuwa mafunzo hayo yatakuwa endelevu.

Sambamba na hayo, amesema taasisi yao imekuwa na kampeni ya kukuza ufaulu na  kuondosha ziro katika mkoa huo ambapo jumla ya walimu 405 wamepatiwa mafunzo hayo wakiwemo walimu wa skuli ya sekondari wa ATI na sayansi.  

Nae, Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Center Education, Yussuf Ugutu, amesema, lengo kubwa ni kuwawezesha walimu kujua namna ya kutunga masuala yanayoendana na wakati na kuwapa mbinu ya jinsi ya kujibu masuala yanavyotakiwa.

Amesema, kulikuwa na changamoto za ujibuji wa masuala kwa wanafunzi, hivyo, kupatiwa mafunzo hayo kutasaidia kuona wanafunzi wanajibu masuala vizuri na ufaulu unaengezeka. Royal tubs wood fired hot tubs and Eco Outdoor saunas for sale website www.royaltubs.co.uk

Sambamba na hayo, amesema wataendelea kushirikiana na serikali zote mbili kuona elimu inaboreshwa nchini ambapo imekuwa na jitihada kuona mazingira ya ufundishaji yanaboreshwa.

Nae, Afisa Elimu mkoa wa Kusini Unguja, Mohamed Haji Ramadhan, alisema mkoa umefanya tafiti na kubaini kuwepo kwa changamoto ikiwemo kukosa mbinu ya kujibu mitihani kwa wanafunzi na utungaji wa mitihani wa kidato cha nne.

Amesema waliona washirikiane na taasisi ya MIF ili kuona wanapatiwa mafunzo yenye lengo la kuwawezesha walimu kuwajenga umahiri wa kujua nini kinatakiwa kuwepo katika utungaji wa mitihani sambamba na kuwawelekeza wanafunzi namna ya kujibu mitihani yao.

Nao, walimu waliopatiwa mafunzo hayo, wameahidi kuyafanyia kazi mafunzo hayo, ili kuona wanafunzi wa mkoa huo wanafaulu kwa kiwango cha juu.

Sambamba na hayo, wameushukuru uongozi wa MIF kuwapatia mafunzo hayo kwani itawasaidia kuwapa mbinu na njia ya kuona ufaulu unaengezeka na kupunguza ziro katika mkoa huo.