Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhammed Mussa amesema wizara ya elimu kwa kushirikiana na  wadau mbalimbali wanaifanyia  tathimini elimu ya Zanzibar ili imuandae mwanafunzi kuweza kukabiliana na hali ya kiuchumi, na fursa mbalimbali za maisha.

Akizungumza katika uzinduzi wa Mafunzo ya  awamu ya pili ya Mradi wa Upimaji wa Stadi za Maisha na Maadili wa Afrika Mashariki (ALiVE) Katika ukumbi wa mikutano golden tulip Malindi Mjini Unguja.

Amesema hatua hiyo ni muhimu kwani kuna Baadhi ya wanafunzi wanamaliza masomo na  kukosa  ujuzi wa kuweza kujiajuri na kuajiriwa.

Amesema uwepo wa  mradi huo utasaidia sana Taifa  kwani Dunia ya Sasa inahitaji wasomi wenye ujuzi wa kivitendo na sio vyeti vya kumalizia masomo pekee.

Mhe Leila ameeleza kuwa Maendeleo ya kielimu yanahitaji bidii za walimu, wazazi na jamii kwa ujumla kwani wao ndio wasimamizi wa wanafunzi ili waweze kubadilika kielimu na kufikia malengo.

Nae Mkuu wa miradi ya Elimu kutoka taasisi ya milele Zanzibar foundation bi Khadija Ahmed sharif amesema mradi huo Wameuzindua  Zanzibar kwa lengo la kuchangia na kuleta mapinduzi ya kielimu nchini.

Ameeleza kuwa awamu ya pili ya mpango huo umewatathimini watoto elfu 45 ili kuchangia maendeleo ya kielimu nchini.

Nae Mkuu wa utafiti wa mradi wa Alive afrika mashariki Dk Jon mugo 
Amesema  tathmini ya ALIVE, inaonesha kuwa  bado vijana wa Africa wanaviwango vya chini sana vya stadi za Maisha na maadili hivyo watashirikiana na vituo vya mafunzo ya ualimu ili malengo. Intellectus ispanų kalbos kursai

Tathmin ya utafiti wa mradi wa elimu umewatathimini watoto kuanzia miaka sita hadi kumi na mbili ili kuweza kuboresha elimu katika nchi za afrika mashariki ikiwemo Tanzania Kenya uganda.

Mafunzo hayo ya siku tatu yamehudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu.