Mkuu wa Divisheni ya Huduman za Wanafunzi, Idara ya Elimu Sekondari, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndg. Suhuba Daudi Issa ameongoza mafunzo maalum ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) kwa wanafunzi wa Skuli za Sekondari kutoka Wilaya mbalimbali za Unguja.
Mafunzo hayo ya siku moja yalifanyika katika ukumbi wa kituo cha walimu (TC) Kiembesamaki Mkoa wa Mjini Magharibi yalilenga kutoa Elimu kuhusu muongozo wa uanzishaji na uimarishwaji wa Klabu za programu hiyo Maskulini kwa jina la “A GUIDE TO CREATE STEM CLUB” kwa wanafunzi wa Sekondari nchini.
Jumla ya wanafunzi wapatao Tisiini (90) walishiriki katika mafunzo hayo yenye lengo la kukuza na kuibua vipaji katika nyanja za Sayansi, uhandisi na Hisabati na kupata wataalamu wazalendo ili kuleta maendeleo ya kweli kwa jamii ya wazanzibari na Tanzania kiujumla.
Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati. Ni mbinu ya kujifunza na maendeleo inayounganisha taaluma hizi ili kuboresha utatuzi wa matatizo, ubunifu na ujuzi mwingine muhimu. Katika muktadha wa elimu, elimu ya STEM inalenga kukuza hamu ya wanafunzi katika nyanja hizi na kuboresha uwezo wao katika uchanganuzi muhimu na utatuzi wa shida.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali - Zanzibar.