Mhe.Lela Muhamed Mussa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar amesema , Wizara itaendelea kushirikiana na Wadau mbali mbali wa Elimu ili kuleta maendeleo bora katika sekta hiyo.
Amesema hayo wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Upishi Salama wa kutumia Gesi katika Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame iliyoko Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema, Wadau wa Elimu kwa kushirikiana na Serikali huleta mabadiliko chanya kwa wanafunzi yatakayo weza kuwasaidia baadae.
Pia Waziri lela ameishukuru Taasisi hiyo na kutoa wito kwa wadau mbali mbali wa Elimu kushirikiana pamoja katika kuunga mkono juhudi Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha utunzaji wa mazingira unafikiwa lengo.
Kwaupande wake Mwenye kiti wa Taasisi ya Mwanamke Intiative Foundation Mhe . Wanu Hafidh Ameir , amesema lengo la Taasisi hiyo ni kutokomeza umasikini na maradhi katika uwekaji wa mazingira yaliyo bora katika upatikanaji wa Elimu kwa
kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri kwa kuacha kwenda kutafutafuta kuni pamoja na kuwaweka wapishi katika mazingira salama.
Amesema, Programu hiyo ya Upishi Salama imelenga kuzifikia Skuli 35 kwa Mkoa mzima wa Kusini Unguja.
Akitoa neno la shukrani Msaidizi Mwalimu Mkuu Ndugu Issa Ameir . Ameishukuru Taasisi hiyo kwa kuandaa programu hiyo na kuwapatia majiko ya gesi na ameahidi kuyatumia vyema ili lengo liweze kufikiwa.
Katika kuendeleza Program ya upishi salama kauli mbiu ni Upishi Salama uwe chachu ya mabadiliko "