Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe.Kyle Nunas amesema Canada itaendelea kushirikiana na kuisaidia Tanzania  hasa katika sekta ya elimu.

Amesema hayo wakati wa ziara maalum ya wenyeviti wa  mabunge  kutoka nchini  Canada ambao ulifanya ziara ya katika skuli ya msingi Mtopepo kuangalia  maendeleo ya mradi wa taaluma  za stadi za maisha unaoendelea katika skuli mbalimbali za Zanzibar  kwa ngazi ya msingi na Sekondari.

Mhe  Kyle amesema Canada  itaka kuona kila mtoto anaelemu ya kujikinga,kujitetea na vitendo vyote vitakavyorejesha nyuma ndoto za maisha yao.

Aidha amesema kila taifa linahitaji  kuzalisha wataalam wazalendo hivyo   watoto  ni lazima wapata taaluma zote hasa ya kujitambua.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgulam Hussein  amesema  kuwepo kwa taaluma ya stadi za maisha kutasaidia taifa kuzalisha wataalam wanaotambia haki zote na wajibu katika maisha yao.

Amesema wizara ya elimu Zanzibar inaelekea katika mageuzi makubwa ya elimu hivyo ni vyema kuwa na vipindi vitakavyowajenga wanafunzi kuweza kujitambua.

Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la kuhudumia watoto  Duniani (UNICEF)nchini Tanzania  bibi Elke Wisch amesema ni jambo la faraja kuona watoto wanapa taaluma  inayohusu kujenga maisha yao.

Ujumbe huo wa Wenyeviti wa  jumuiya ya mabunge Canada  uliongozwa na balozi wa Canada nchini Tanzania umefika katika skuli ya msingi Mtopepo  ikiwa ni darasa  mfano kupia mradi huo.

Mradi wa wa kuwapa taaluma ya stadi za msisha unatekelezwa na Serikali ya Canada kupitia shirika la kuhudumia watoto Duniani (UNICEF)